Bure Muziki Kuzuia Watoto Kuzuia Programu
Ningetaka kuwaleteeni mpango wa Mwili Wangu Ni Mwili Wangu. Huu ni mpango unaolenga kuzuia Dhulma dhidi ya watoto kwa kutumia nyimbo na uhuishi, ambao hutoa njia mbadala ya kukabiliana na mada hii ngumu kwa njia ya furaha, uhuishi na nyimbo.
Matokeo ya dhulma dhidi ya watoto kwa mtoto mhusika na pia kwa jamii huwa makuu, na elimu ni mojawapo ya njia bora zaidi za kuzuia.
Tukio hili, ama angalau; endapo tayari mtoto anadhulumiwa,
itampa maarifa ya kujua atakachokifanya na wa kumwendea ili kupata usaidizi.
Ni bora zaidi Tunapo wafunza watoto mapema kuhusu “Usalama wa Mwili”, nina uhakika kuwa mpango huu ni wenye mafankio kwa watoto wenye umri wa miaka 3 na zaidi, kwani nimeuwasilisha kwa zaidi ya watoto 350,000 nchini Marekani kwa mafanikio makubwa.
Uzuri wa mpango huu wa Mwili Wangu ni Mwili Wangu ni kuwa yeyote anaweza kuufunza. Wafanyakazi wa jamii, waalimu, waalimu wa chekechea, wazazi, wakurugenzi wa vilabu vya michezo na wengine wengi. Mpango huu sio mgumu, ni usiosahaulika, na hufungua njia za mawasiliano kuhusiana na suala la dhulma, suala ambalo lina umuhimu mwingi sana.
“Je, utawaendea vipi watoto wachanga kuhusu suala la dhulma dhidi ya watoto?”
Idadi kubwa ya watu wazima hawapendi kulizungumzia suala la dhulma dhidi ya watoto , na dhana ya jaribio la kuwaendea watoto wachanga kwa njia mwafaka huenda ikawa matarajio magumu. Nyimbo za furaha zilizoko kwenye mpango huu huwawezesha watu kuwahusisha watoto kwa njia rahisi na mwafaka.
Mbona Muziki?
Nyimbo pia ni njia mwafaka ya watoto kukumbuka jumbe muhimu zinazowasilishwa kwao kwani nyimbo huwashirikisha. Nina uhakika kuwa nyote mwakumbuka nyimbo chache mlizofunzwa mlipokuwa watoto, nyimbo hizi na jumbe zitaishi na watoto hao na pia zitakuwa msingi mwema wa mafunzo ya maisha katika siku za usoni.
Utafiti uliowahusisha watoto, na kuchapishwa kwenye jarida la Music Therapy, ulionyesha kuwa muziki, na kusoma nyimbo mpya kunahusiana na kujielewa vyema Zaidi na ukuzaji wa hisia ya kujiheshimu,
na vile vile huwasaidia watoto wawe na hisia njema kujihusu.
*The Power Of Music – University of London
Jinsi Ya Kutumia Mpango huu:
Ufanye Kwa furaha –
Nyimbo hizi ni uigizaji wa kufurahisha, unaoletwa kwako na mhusika kibonzo aitwaye Cynthie. Imbeni pamoja naye, fanya ishara za mikono, chezeni, fanyeni lolote ili kuhakikisha kuwa ujumbe hautasahaulika.
Ufanye kwa urahisi –
Watoto wachanga hawahitaji kujua maelezo kuhusu dhulma
“kwa undani”, wape maagizo rahisi:
1. Hakuna mtu yeyote anayefaa kukuumiza
2. Hakuna mtu yeyote anayefaa kuzishika sehemu zako za siri
3. Hakuna mtu yeyote anayefaa kuzipiga picha sehemu zako za siri
4. Endapo una tatizo lolote mwambie mtu
5. Usiweke siri iwapo kuna mtu yeyote anayekuumiza au
kuzishika sehemu zako za siri
6. Mwambie mtu iwapo kuna yeyote anayekudhulumu
Weka Kuwa Mzuri –
Lengo kuu ni kuwatia moyo watoto ili wawe na hisia njema kuihusu miili yao, na usalama wakiwa na maarifa
Lengo kuu ni kuwatia moyo watoto ili wawe na hisia njema kuihusu miili yao,
na wajihisi wako salama huku wakijua kuwa wana mtu wa kuzungumza naye iwapowana shida yoyote.
Nakala hii imeandikwa na kuhuishwa na
Chrissy Sykes © 2017
Tafsiri : JB Mugi
Music Studio Sponsored by Stichting GetOn
Song 1
Wimbo wa kwanza Mwili Wangu Ni Mwili Wangu
"
Nakala ya Cynthie toka kwenye video Hamjambo, jina langu ni Cynthie na leo tutafanya mpango wa “Mwili wangu ni Mwili wangu”. Tutaimba nyimbo kadhaa, tufurahie na tusome kuhusu jinsi ya kukaa salama. Mnajua, miili yetu ni maalum sana na hakuna mtu anayefaa kutuumiza, ama kushika sehemu zetu za siri ama kufanya jambo lolote la kutupatia wasiwasi kwa sababu ni mwili wetu maalum. Tutaimba wimbo wetu wa kwanza sasa – na nataka pia nanyi muimbe pamoja na mimi – Unaitwa mwili wangu ni mwili wangu
"Song 2
Wimbo wa pili Iwapo Huna Hisia Njema Kulihusu, Usilifanye!!
"
Nakala ya Cynthie toka kwenye video Tutafurahia wimbo huu unaofuata, una kanuni kuu ya kukumbukwa Na kanuni hiyo ni – kama linakupa wasiwasi – usilifanye!! Sasa siongei kuhusu mambo kama vile kufanya kazi yako ya ziada, ama kusafisha chumba chako cha kulala. Naongea kuhusu kama mtu anajaribu kukufanya uende mahali popote na yeye na unajua kwamba sio jambo nzuri kufanya. Kama linakupa wasiwasi – usilifanye!! Ama ikiwa mtu anajaribu kukufanya ufanye jambo ambalo linakutia wasiwasi. Kama linakupa wasiwasi – usilifanye!!
"Song 3
Wimbo wa Tatu Tutacheza mchezo wa “nini iwapo”
"
Nakala ya Cynthie kutoka kwenye video Sasa tutacheza mcheza wa “nini kama” na katika wimbo huu tutasoma cha kufanya iwapo mgeni atajaribu kukufanya uende naye, ama kama mtu atajaribu kushika sehemu zako za siri. Je unajua sehemu zako za siri ziko wapi? Ziko sehemu ambayo nguo zako za ndani hufunika. Hakuna mtu anayefaa kuzishika sehemu zako za siri acha tu wakati wewe ni mchanga sana, baba ama mama atakuosha hapo, lakini punde utajua kujiosha mwenyewe. Ama labda wewe ni mgonjwa, Baba ama Mama ama Daktari huenda akakupaka dawa hapo, lakini mbali na hayo hakuna mtu anayefaa kuwa akizishika sehemu zako za siri. Pia tutasoma cha kufanya iwapo mtu wa familia yenu ama nyumbani kwenu atakufanya upatwe na wasiwasi ama ajaribu kukuumiza. Kila unachofaa kufanya katika mchezo huu ni kukataa kwa sauti “hapana” kwa hivyo nataka useme vizuri kwa sauti
"Song 4
Wimbo wa Nne Iwapo una shida
"
Nakala ya Cynthie toka kwenye video Ni muhimu sana kumwambia mtu kama mtu anakuumiza ama anakugusa sehemu za siri, hata kama unaogopa ama kuona aibu unafaa kuwa na ujasiri mwingi na kumwambia mtu. Kuna watu wengi wa kuwaambia, Mama, Baba, Bibi, Babu, shangazi, wajomba, waalimu, binamu, majirani, wazazi wa rafiki zako, polisi, wauguzi na watu wengine wengi walio karibu na wewe. Sasa ukiwaambia na watu wakose kukwamini, huenda hata wakakwambia uliweke kama siri – lakini nenda ukamwambie mtu mwingine. Iwapo hatakuamini – nenda ukamwambie mtu mwingine na uendelee kuwaambia hadi mtu atakapo kusikiliza. Usikufe moyo
"Song 5
Wimbo wa tano Upendo ni mpole
"
Nakala ya Cynthie toka kwenye video Tuongee kuhusu upendo, ni jambo la muhimu sana kupendwa na watu hawakuoneshi upendo wao kwako kwa kukuumiza ama kwa kufanya mambo ambayo hukupatia wasiwasi. Watu huonyesha kuwa wanakupenda kwa kufanya mambo pamoja na wewe kama vile kusoma vitabu, kucheza michezo, ama kufurahia, kuenda matembezi ama kukufunza jinsi ya kuendesha baiskeli. Upendo ni kusaidiana na kujaliana. Wazazi wetu na wanaotuchunga huhakikisha kuwa tumelindwa, hutupatia chakula, huhakikisha kuwa tumepiga meno mswaki na kuwa tuna nguo safi za kuvalia na iwapo tu wagonjwa wao hutupeleka kumwona daktari. Ni muhimu sana kuwa tunalindwa vizuri ili tuweze kukua kwa afya, furaha na tupate nguvu.
"Signs of Child Abuse
Ishara za dhulma dhidi ya watoto
Zifutazo ni ishara za dhulma au upuuzaji ambazo huenda ukaziona na watoto. Iwapo utaziona ishara hizi ama mtoto akujulishe jambo Fulani:
1. Kuwa mtulivu na usimlazimishe akuambie zaidi.
2. Mfariji mtoto huyo na umshukuru kwa ajili ya kukujulisha, kisha uyajulishe Mashirika husika ya Huduma za Kuwalinda Watoto.
3. Kumbuka kuwa mtoto huenda akakupa tu asilimia ndogo ya habari kila wakati hadi watakaporidhika kuwa wewe ni mtulivu na unampa usaidizi.
Zifuatazo ni ishara za dhulma. Huenda mtoto anatatizika na baadhi ya dhulma hizi hivyo basi huu ni mwongozo tu. Endapo utatambua mabadiliko makuu katika tabia za mtoto hakikisha kuwa umeyazingatia na uone iwapo yafuatayo yanalingana.
Ishara za dhulma za kimwili.
Anavyoonekana mtoto.
*michibuko isiyo ya kawaida, lengelenge, kuvunjika
*alama za meno katika sehemu alizoumwa
*majeraha ambayo husingiziwa kutokana na ajali
*endapo maelezo hayatalingana na jeraha
*kuvalia mavazi marefu ili kuficha majeraha tabia ya watoto
*asiyeeleweka
*wenye woga usio wa kawaida, na huwaepuka watu wengine
*aliye na hamu kuu ya kuwapendeza wengine
*aonekanaye kuwaogopa wazazi
*aonekanaye kutojali anapotenganishwa na wazazi.
Ishara za kupuuzwa
Aonekanavyo mtoto
*mchafu, nywele chafu,
*anukaye vibaya
*aliye na mavazi yasiyoambatana na hali ya anga
*anayehitaji matibabu
Tabia ya mtoto
*aliye na uchovu kwa wakati mwingi
*aliye na tabia ya kuba au kuomba chakula
*akosaye kuenda shuleni siku nyingi au achelewaye wakati mwingi
*mtoto asiyetii amri
*asiyejiamini o
Ishara za dhulma za Hisia
Aonekanavyo mtoto
Huenda ishara hizi zikakosa kuwa bainifu kama zilivyo katika hali zingine, tabia huenda zikawa ishara bora zaidi.
*kujitenga na marafiki
*akosaye kuenda shuleni siku nyingi au achelewaye wakati mwingi
*asiyejiamini
*asiyetii amri
*mabadiliko katika masomo yake
Ishara za dhulma za kingono
Aonekanavyo mtoto
*mavazi ya ndani yaliyoraruka na yenye matone ya damu.
*anayehisi uchungu katika sehemu zake za siri
*aliye na magonjwa ya zinaa
Tabia za mtoto
Kwimbonakalo yomntwana
*tabia za kingono au maarifa ambayo yasiyolingana na umri wake
*kuwashika watoto wengine kwa njia isiyofaa
*mabadiliko ya ghafla ya tabia
*kuzuia vikali kushikwa kwa njia yoyote ile
Endapo utashuku dhulma dhidi ya mtoto, yajulishe Mashirika husika ya Huduma za Kuwalinda Watoto ili kupata ushauri unaofaa. Watayasikiliza matakwa yako na kuchukua hatua kwa niaba yako iwapo mtoto yu hatarini.
Tuwalinde watoto!!
Nakala hii imeandikwa na kuhuishwa na Chrissy Sykes © 2017
Tafsiri : JB Mugi
Maswali ambayo huulizwa sana (na watoto)
Swali: Mbona watu huwaumiza watoto?
Jibu: Kuna baadhi ya sababu za watu kuwaumiza watoto, baadhi yao waliumizwa walipokuwa wachanga pia na kuendeleza Tabia hiyo ya kuwaumiza wengine. Watu wengine huwa na matatizo ya ulevi, mihadarati au hasira na hivyo basi kuwaumiza watoto. Jambo kuu la kukumbuka ni kuwa ni vibaya kuwaumiza watoto na kwa sababu hiyo kuna haja ya kumwambia mtu, ili upate usaidizi.
Swali: Mbona watu huwashika watoto sehemu zao za siri?
Jibu: Tena, kuna sababu nyingi ambazo huwafanya watu kuwadhulumu watoto kingono, watu wengi ambao huwadhulumu watoto pia wao walidhulumiwa na kwa sababu hiyo ni muhimu kumwambia mtu, kwani watu wa aina hiyo wanahitaji usaidizi na matibabu ili wawe watu wema na kuacha kuwaumiza watoto tena.
Swali: NIfanyeje iwapo hakuna yeyote atakayeniamini?
Jibu: Endapo utamwambia mtu na akose kukuamini- basi mwambie mtu mwingine hadi utakapompata mtu atakayekuamini.
Swali: Nikimwambia mtu, nini kitafanyika?
Jibu: Watahitajika kupiga ripoti kuwa unaumizwa. Kisha mtu atakuja na kuzungumza na famila yako. Wataona iwapo iatakuwa salama kwako kukaa nyumbani ama unahitaji kuenda mahali kwingine utakakokuwa salama.
Swali: Nitafanyaje iwapo nitasema HAPANA!! Nao wazidi kusisitiza?
Jibu: Wasipokoma unaowaambia hapana- itana kwa sauti iwapo kuna mtu ambaye anaweza kupa usaidizi, au ukijua kwamba kuna watu ambao wanaweza kuja kukupa usaidizi. Endapo hakuna yeyote, basi nenda kamwambie mtu punde itakavyokuwa salama kufanya hivyo
Swali: Nitafanyaje iwapo wataniambia kuwa wataniumiza au mtu mwingine katika familia yangu endapo nitasema?
Jibu: Watu ambao huwadhulumu watoto hawapendi watu wengine wanapojua wanachokifanya, hivyo basi huenda wakajaribu kukutishia au kumtishia mtu mwingine yeyote katika familia yako na kukuambia uweke jambo hilo kama siri. Unafaa kuwa na ujasiri mwingi na umwambie yeyote kuihusu shida yako.
Swali: Nitafanyaje endapo nadhulumiwa na kaka yangu au dada yangu?
Jibu: Waambie wazazi wako na wasipo kusikiliza mwambie mtu shuleni au yeyote aliyekuwa kwenye orodha ya watu tuliyoijadili hapo awali.
Swali: Je watakasirika nikiwaambia?
Jibu: Sio kila wakati, lakini huenda wakashikwa na hasira, lakini bado unafaa kuwa na ujasiri na uwaambie ili anaykudhulumu akome kukuumiza au kuzishika sehemu zako za siri.